(Fully Registered by NACTE, with Reg. No PEG/BMG/030)
P. O. Box 2482 Dodoma: Tel: 026–2301425 Mobile:0754 272036
Web Site: www.aseki.ac.tz Email:asekibs@aseki.ac.tz
TANZANIA
Download Advert in Portable Document Format (PDF)
and Application form for 2013/2014
KARIBUNI ASEKI BUSINESS SCHOOL
ASEKI Business School ni chuo kipya kilichoanzishwa mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka jana 2010. Chuo kipo eneo la Miyuji, kadiri ya kilomita 3 kutoka katikati ya jiji la Dodoma kuelekea njia ya Arusha. Ingawa Chuo cha ASEKI bado ni kipya na kichanga lakini kina huduma zote muhimu. Yapo madarsa ya kisasa na nadhifu, maktaba nzuri inayotosha kukaa zaidi ya wanafunzi 60 kwa mpigo. Kuna maabara ndogo ya kompyuta na Kafeteria ya chakula cha wanafunzi na wafanyakazi.
Chuo kimeshashapata Usajili Kamili kutoka NACTE; Namba ya usajli ni PEG/BMG/030. Hii ina maana mtu yeyote atakayesoma ASEKI na kufanikiwa kupata cheti, cheti hicho kitatambuliwa rasmi nchini Tanzania na Dunia kote. Kwa sasa chuo kinaendesha kozi kwa ngazi ya Cheti na Diploma kama ifuatavyo:
Kozi ya Cheti
Madarasa mapya ya ngazi ya Cheti (NTA – 4) yataanza tarehe 16-03-2013 katika fani tatu zifuatazo
- Basic Technician Certificate in Accountancy
- Basic Technician Certificate in Business Administration
- Basic Technician Certificate in Procurement and Supply.
- Basic Technician Certificate in Marketing
Kozi ya Cheti ni ya mwaka mmoja. Atakayefaulu vizuri kozi hii atajiunga moja kwa moja na kozi ya Diploma ya miaka miwili. Mwanafunzi yeyote aliyemaliza Kidato cha Nne na kupata angalau D tatu (3) anaweza kujiunga na kozi hii. Karo kwa kozi ya cheti ni sh800 000 tu kwa mwaka
Kozi ya Diploma
Madarasa mapya ya kozi ya Diploma yataanza tarehe 7 May 2012 katika kozi fani tatu, yaani
- Diploma in Business Administration (NTA 5 – 6)
- Diploma in Accountancy (NTA 5 – 6)
- Diploma in Procurement and Supplies (NTA 5 – 6)
Karo kwa ngazi ya Diploma ni sh 900 000 tu kwa mwaka.
Mwanafunzi yeyote aliyemaliza kozi ya cheti (NTA 4) inayoendana na fani hizi kutoka kwenye chuo chochote kingine kilichosajiliwa na NACTE au aliyemaliza Kidato cha Sita na kupata angalau Principal Pass moja au Subsidiary pass mbili anaweza kujiunga na kozi ya diploma.
Hosteli: Tuna nafasi chache za Hosteli kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Dodoma kwa gharama ya sh350 000 kwa mwaka.
Wewe mzazi au mlezi kama una kijana au binti aliyemaliza Kidato cha Nne na amekosa sifa ya kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano, usikate tamaa. Ili mradi amefaulu na kupata angalau pasi (D) tatu, mlete ajiunge nasi. Sisi tutampa sifa ya kuweza kujiunga na Chuo Kikuu chochote hapa nchini ndani ya miaka mitatu tu. Aidha, tutampa Stadi za kumuwezesha kujiajiri mwenyewe au kuajiriwa baada ya miaka hiyo mitatu ya kwanza endapo atashindwa au ataamua kutoendelea na masomo zaidi
Fomu za kujiunga na chuo zinapatikana katika ofisi zetu zilizopo Miyuji mjini Dodoma, au pakua kutoka kwenye Tovuti yetu. Kwa taarifa zaidi tembelea Tovuti yetu, www.aseki.ac.tz
Wasifu
Mimi ninayewaalika ni mwanataaluma mwenye uzoefu wa miaka mingi katika tasnia ya Elimu ya Juu, hususan Elimu ya Biashara. Nina shahada ya ualimu wa masomo ya sayansi [BSc (Ed)] ya mwaka 1979, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili ya Uedeshaji Biashara (MBA) ya mwaka mwaka 1998, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nimefundisha Chuo cha Elimu ya Biashara kwa miaka 31 na kustaafu mwaka 2010. Miaka 21 ya mwanzo nilikuwa Makao Makuu ya CBE Dar es Salaam. Miaka 10 ya mwisho nilipewa dhamana ya kuwa Makamu Mkuu wa Chuo nikisimamia Kampasi ya Dodoma. Katika kipindi cha uongozi wangu, CBE Dodoma ilipata mafanikio makubwa sana. Inatosha tu nikisema nilipokea chuo kikiwa na wanafunzi 183 na nikakiacha kikiwa na wanafunzi zaidi ya 4000. Nyongeza hii ya wanafunzi imeleta mabadiliko makubwa sana CBE Dodoma. Kwa vile nilifanyakazi kwa bidii, utiiifu, ubunifu na uadilifu mkubwa, nilipostaaafu, mwajiri wangu alinipa zawadi nyingi, ikiwemo Cheti cha Utumishi wa Umma Uliotukuka. Hivyo nawahimiza wazazi na walezi wote, “ leteni watoto wenu kwangu ili waendelee kufaidi utumishi wangu uliotukuka”.
Karibuni sana
Omari M. Kiputiputi
Principal and Co founder